Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 7. März 2012

TZMPAKAAU

WANAWAKE KUFANYA MAOMBI MAALUM KWA TAIFA MARCH 8.
(WOMEN DECIDE TO DO SPECIAL PRAYERS FOR THE NATION,ON WOMEN'S DAY)
Deborah E.Mallasy with her husband Geodfrey E.Mallasy
Wanawake wa madhehebu mbalimbali jijini Dar es Salaam wameamua kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2012 kwa kufanya maombi maalum ajili ya Taifa la Tanzania. Maombi hayo yatafanyika Machi 8, 2012 katika ukumbi wa Sinza Christian Centre jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni hadi saa 1.00 usiku.
Kwa mujibu wa muandaaji wa maombi hayo ya kitaifa, Mchungaji Deborah Malassy wa kanisa la Tanzania Fellowship of Churches (TFC), maombi hayo yanafanyika ili kuliombea Taifa, ndoa na familia ili Mungu aweze kuzidisha ulinzi wake.
“Maombi haya ya Wanawake Waombolezao Kitaifa kutoka makanisa mbalimbali, yatawashirikisha akinamama wa kada tofauti na tumeamua kuadhimisha siku hii maalum kwa njia ya maombi kwa kuliitia jina la Yesu kwa ajili ya Taifa letu, kanisa, huduma zetu, ndoa zetu, familia zetu na uchumi wetu binafsi na wa Taifa kwa jumla,” alisema.
Vyanzo:TZMPAKAAU na thehabari

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen