Best Blogger TipsSoon

Samstag, 10. März 2012

TZMPAKAAU

ARUMERU NI JOSHUA NASSARI TU:CHADEMA
(Kushoto ni Joshua Nassari mgombea wa CHADEMA Arumeru na  kulia ni mbunge wa CHADEMA Joyce Mukhya.)
Chama cha CHADEMA kimefanya uzinduzi wa kampeni zake za ubunge kwa jimbo lililoachwa wazi la Arumeru kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Jeremiah Sumari.
Chadema imefanya uzinduzi huo kwa maandamano yaliyoanzia Arusha mpaka Arumeru na maandamano mengine yakianzia Kia hadi Arumeru maandamano hayo pia yangerushwa na kituo cha Televisheni cha Star TV moja kwa moja.Akihutubia kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo mwenyekiti wa CHADEMA taifa bw.Freeman Mbowe alisema" uchaguzi huo sio wa Meru pekee bali una sura ya kitaifa.Taifa zima linafuatilia Arumeru Mashariki kujua mnafanya nini, nawaomba sana mtuchagulie Joshua Nassari ili mtuongezee nguvu bungeni dhidi ya chama cha magamba kwani mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 30 wa CCM”.
(Star TV walikuwepo kurusha matangazo ya tukio moja kwa moja.)
Naye mgombea wa jimbo hilo Joshua Nassari alisema,"kwa upande wake Nassari aliomba wakazi wa Meru wamtume kuwa mbunge ili awatetee ardhi yao, inayomilikiwa na wachache, asaidie kushughulikia tatizo la maji, ajira kwa vijana na masoko ya uhakika ya bidhaa mbalimbali, ikiwepo soko la kila wiki la Mbuguni".
( Maandamano ya CHADEMA kutokea Arusha yaliyokuwa na mamia ya pikipiki pamoja na magari yaliongozwa na mbunge wa Arusha mjini kamanda Godbless Lema na huku maandamano yaliyotokea KIA yakiongozwa na mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa.)
(Arusha sio wanawake ,sio wanaume sio vijana, sio wazee,sio watoto swala la siasa sio la wanasiasa sio swala la CCM au CHADEMA ni swala la jamii nzima kwaiyo hakuna anayebaki nyuma.)
(Kama ulikuwa huamini maneno ya TZMPAKAAU basi bibi na kijana wote walikuwa wakisubiria kuona uzinduzi wa kampeni ubunge za CHADEMA  arumeru.)
(Basi TZMPAKAAU haiongezei maneno.)
Mbunge wa CHADEMA Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe yeye aliwaomba wananchi wa Arumeru kuenzi msingi ulioasisiwa na wazee wao kwa kusimama kutetea haki dhidi ya uonevu akitaja tukio la mwaka 1951 walipochanga fedha na kumtuma Mzee Japhet Kirilo kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), kudai ardhi ya Meru iliyokuwa ikikaliwa na walowezi wa kikoloni.

(Barabara zilizazimika kufungwa kwa muda kuruhusu msururu wa magari na pikipiki za CHADEMA.)
(Wananchi wa arusha na wapenzi wa CHADEMA kama walivyonaswa na kamera)
(Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama taifa CHADEMA ,bw.Lwakatare katikati)
Mbunge wa Arusha kamanda Godbless lema alipopokelewa na wananchi wa Arusha kwa kubebwa juu juu.)
(Mbunge wa Karatu CHADEMA na meneja wa kampeni za Arumeru mchungaji Yohana Natse)kulia.
()Maelezo ya picha husika.
Vyanzo:TZMPAKAAU,MWANANCHI,MJENGWA na the habari.



Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen