NCCR Mageuzi yataka waziri Mponda na Nkya wajiuzulu(NCCR Mageuzi calls minister of health and social welfare and his deputy to resign)
Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samuel Ruhuza, amesema kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyosema kwamba kuwataka Waziri wa Afya Dk. Khaji Mponda na Naibu wake Lucy Nkya, wajiuzulu ni kuwaonea kwa sababu hawana muda murefu katika wizara hiyo, haina hoja ya msingi.Ruhuza alisema“Suala la kujiuzulu kwa kiongozi ni uwajibikaji, ambao unakuja baada ya kiongozi husika kuona kwamba hakubaliki katika eneo lake au endapo kumejitokeza jambo la kupishana kimawazo au kiutendaji".Kadhalika, Ruhuza aliwataka madaktari hao kutathmini athari za mgomo na kuwaonea huruma wananchi, licha ya kwamba wana haki ya kudai haki yao.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia na Nyakasagani
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen