Best Blogger TipsSoon

Sonntag, 19. Februar 2012

TZMPAKAAU

TANZANIA,COMORO NA USHELISHELI ZAWEKA MIPAKA MIPYA YA BAHARI.

Serikali za Tanzania, Ushelisheli na Comoro zimesaini Mkataba wa Makubaliano ya Mpaka wa Bahari ya Hindi baina nchi hizo.
Utiaji saini huo ulifanyika Februari 17, mwaka huu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, mjini Mahe.
Katika hafla hiyo, Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Ushelisheli iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Jean-Paul Adam; na Comoro ilimtuma Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano, Mohamed Ben Charif.


Vyanzo:TZMPAKAAU na Mjengwa

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen