- Waziri Mkuu wa Zimbabwe amesema uhusiano wake na mfanyabiashara Leocadica Tembo umefikia tamati siku chache baada ya kutoa mahari
Waziri mkuu bw .Morgan Tsvangirai (59)ambaye mke wake bi Susan Tsvangirai alifariki muda mfupi baada ya Morgan kuwa Waziri Mkuu...anasema kuna mkono wa kisiasa nyuma ya mahusiano yake na Leocadica .Bi Leocadica Tembo (39) ni mfanyabiashara na ni dada wa mbunge mmoja kutoka chama cha bw. Mugabe cha Zanu-PF.Katika taarifa iliyotolewa na waziri Mkuu huyo inasema anatia shaka kama ndoa yao itakuwa na umoja thabiti.Mahusiano haya yamegubikwa na mambo mengine, na kuna mkono wa kisiasa hapa, Waziri aliongeza "nimekuwa mtizamaji katika uhusiano huu na mambo yanaenda haraka sana kwenye kamera bila mimi kufahamu. Hii inanifanya niamini kuna njama nzito nyuma ya mahusiano yetu na hii imeniondoa imani"alimaliza.
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen