Best Blogger TipsSoon

Freitag, 12. August 2011

TZMPAKAAU


Afrika Kusini yaidhinisha bima ya afya


Afrika Kusini imepiga hatua katika kuimarisha afya ya umma, baada ya serikali kuridhia bima ya afya ya kitaifa.
Bima hii inanuia kumwezesha kila raia wa Afrika Kusini kupata matibabu.
Waziri wa afya Aron Motsoaledi ametangaza mpango huo wa bima ya afya baada ya baraza la mawaziri kuuwidhinisha kwenye kikao cha Jumatano. Umma utakubaliwa kutoa maoni yao juu ya bima hiyo kabla ya mswada wake kuwasilishwa bungeni.

Waziri huyo amesema bima hii itaanza kutekelezwa kwa awamu kwanzia mwaka ujao na kuendelea hadi miaka 14. Bima hii inatoa nafasi kwa maelfu ya raia masikini wa Afrika Kusini kuweza kupata huduma bora za matibabu, kwa gharama ya chini sana

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen