Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 4. August 2011

TZMPAKAAU

Waziri Nundu Hoi
  • Wabunge wa CCM upinzani waungana kuikataa bajeti
  • Skadi za Mbowe,Mdee,Zambi,Kizeba zamuweka pabaya
 
Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, anaelekea kukwama sawa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, baada ya Wabunge kuiikataa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 na kutaka irejeshwe serikalini ili kufanyiwa maboresho yatakayoleta tija katika usafiri wa reli, meli na ndege.
Pia wametaka Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Bakari Kingobi, wakurugenzi wa UDA kukamatwa ili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa mali za umma uliofanywa katika shirika hilo.
Wakichangia hotuba ya makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa nyakati tofauti bungeni jana, wabunge hao walisema Sh. 237,563,802,000, zilizotengwa ni finyu na vigumu kuboresha huduma za usafiri wa anga, majini na reli nchini.
 
Kwa habari zaidi tembelea Ippmedia
Vyanzo:Ippmedia,TZMPAKAAU



Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen