Best Blogger TipsSoon

Montag, 25. Juli 2011

TZMPAKAAU

  Mbunge aikejeli CCM kwa kushindwa kumaliza umaskini

                       
                                        Mbunge wa kilwa kusini bw.Selemani Bungara

MBUNGE wa Kilwa Kusini, Bw. Selemani Bungara (CUF), ameikejeli Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiishukuru kwa kushindwa kuondoa maadui wa
maendeleo katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.

Akichangia hotuba ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, mbunge huyo alisema wakati taifa linaelekea kusherehekea miaka 50 ya uhuru bado, CCM imeshindwa kuondoa ujinga, maradhi na umaskini hali inayowafanya wananchi kuelemewa na mizigo.

“Miaka 50 ya Uhuru bado hatujaweza kujitegemea, Mwalimu Nyerere alisema asiyeweza kujitegemea hayupo huru, mpaka sasa asilimia 87 ya bajeti hii tunategemea wafadhili, tunaishukuru serikali ya CCM kwa kutufikisha hapa tukiwapa miaka mingine 50 watatufikisha kubaya zaidi,” alisema Bw. Bugara.



Akizungumzia juu ya wakulima wa ufuta Kilwa, mbunge huyo alisema viongozi wa serikali mkoani humo wamekuwa wakiwazuia kuuza zao hilo kwa bei nzuri na kuwapongeza viongozi hao kwa kuwapa nguvu wapinzani.

“Sisi watu wa Kilwa tunaonewa sana, wakulima wanapanda wenyewe, wanapalilia wenyewe, lakini wakianza kuvuna serikali inakuja na kuwataka kuuza kwenye vyama vya ushirika ambako ni sh 1,000 kwa kilo na kuwakataza kuuza kwingine ambako ni sh 1,500,” alisema mbunge huyo.

“Hayo ndio matunda ya CCM. Nilimwandikia barua Waziri Mkuu, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika na Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya kuwa wakulima wa Kilwa wanaonewa, sijajibiwa mpaka leo aliongeza.
Vyanzo:Majira,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen