Best Blogger TipsSoon

Montag, 25. Juli 2011

TZMPAKAAU

   Samaki kutoka Fukushima wakamatwa Dar

Shehena ya samaki wanaohofiwa kuwa na mionzi ya nyuklia imekamatwa katika soko la Kimataifa la samaki la Feri jijini Dar es Salaam, ikiwa tayari kwa kuuzwa

Samaki hao ambao walikuwa ndani ya maboksi 50 walikamatwa jana majira ya saa 2:00 na Jeshi la Polisi wakishirikiana na maofisa kutoka Ofisi ya Mkemia wa Serikali.

Walioshuhudia tukio hilo, walisema katoni hizo za samaki aina ya Kamongo zilikamatwa mara baada ya kushushwa na kampuni moja ya jijini (Jina linahifadhiwa) kwa ajili ya kuwauzia wananchi wanaofika sokoni hapo.

Mfanya biashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Juma Ramadhani alisema alishuhudia maofisa hao pamoja na askari wakichukua maboksi hayo yaliyoletwa hapo kwa ajili ya kuwauza.
“Tulishtukia watu wakivamia na kuchukua katoni zote zilizoletwa na kutuambia hazitakiwi kuuzwa mpaka ifanyike uchunguzi,” alisema Ramadhani.

Afisa mmoja wa Uvuvi wa Manispaa ya Ilala ambaye hakutaka jina lake litajwe, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa hawakujua kama samaki hao walitoka nchini Japan sehemu iliyoathirika na mionzi ya nyuklia.

Samaki hao walifikishwa Bandari ya Dar es Salaam wiki tatu zilizopita wakitokea katika bahari ya Fukushima ambapo kulitokea maafa ya vinu vitatu kulipuka na kusababisha nyuklia kuvuja.
 
Vyanzo :TZMPAKAAU,NIPASHE

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen