Best Blogger TipsSoon

Samstag, 25. Juni 2011

TZMPAKAAU

This week in pictures




Mama Michelle Obama ijumaa alipokuwa botswana alikaribishwa na ngoma Mama Michelle ametembelea klinik za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini botswana
Wa Syria bado wameendelea kushikilia msimamo wao hawamtaki Bashar Al Assad,lakini yeye anasema suluhisho ni kukaa na kumaliza tofauti zao.

Czech Slovakia wiki hii waliazimisha mwisho wa utawala wa Urusi baada ya vita vya pili vya dunia kwa kukipaka kifaru rangi hiyo.

Hii ni black hole mimi ,sina utaalamu zaidi ila unaweza ukatafuta taarifa zaidi kuwa hii ni nini hasa?

Wagiriki wiki hii walipiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu wao bw George Papandreou,kutokana na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo.

Mafuriko makubwa yanaendelea nchini china,watu 130 wamepoteza maisha zaidi ya watu laki nane hawana makazi, watu zaidi ya 10,000,000 wamepoteza mali wameumia au wanateseka kutokana na kukosekana kwa huduma muhimu kama maji,umeme,chakula na miundo mbinu

Hizi ni kambi mpya za wakimbizi zilizoanzishwa nchini uturuki kuwahifadhi maelfu ya wakimbizi wanaotoka nchi jirani ya Syria
Huyu mtoto ana miaka nane anaitwa Raby akiwa mjini Wau southern Sudan kama mkimbizi kutoka jimbo linalogombewa la Abieyi wazazi wake wapo wapi,kaka zake,dada zake,anakula nini,analala wapi Mungu ndiye anayejua.

Benghazi vita imekuwa sehemu ya maisha,lakini ukiacha mzaha watu wengi sana wanapoteza maisha hali inatisha sana nchini Libya sasa kuna makaburi yasiyo na idadi,ukiachilia mbali uharibifu ambao hata wewe ni shahidi.
Waziri mkuu anayejua nini maana ya maisha....waziri mkuu wa Italia bw.Silvio Berlusconi ana kesi zinazomkabili,chama chake kimeshindwa mfululizo na wapinzani,hali ya uchumi ni mbaya hapa anakunywa Capuccino  katikati ya kikao cha serikali.


Komandoo wa Brazil akiwa mazoezini,Brazil ni nchi ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi, hivyo nchi hiyo kwa upande mwingine inajiimarisha zaidi na zaidi kijeshi kama zifanyavyo nchi kama China,India,Uturuki na nyenginezo

Wanamieleka wa kipakistani kama walivyokutwa na kamera katika mazoezi yao ya kila siku mchezo wa mieleka ya aina hii unahistoria ndefu nchini pakistani

Baada ya miaka kumi ya kupambana sasa ni muda wa kulala tu,hawa ni wanajeshi wa Canada nchini Afaghanistan jimbo la Kandhar wanajeshi wa Canada wanaondoka nchini Afghanistani mwezi ujao baada ya kupambana kwa zaidi ya miaka 10 na wataleban.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen