- Ashauri maoni ya wananchi yasikilizwe na yazingatiwe
- Asema EAC ijifunze toka EU(European Union) iliyochukua miaka 10 kuwa na Euro
Rais wa zamani wa ujerumani Hörst Kholer
Profesa Kohler aliyasema hayo, wiki iliyopita, mjini Arusha, kwenye mdahalo maalumuwa kuangalia Matarajio na Uhalisia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika Ulimwengu wa Utandawazi. Mdahalo huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwemo wanadiplomasia kadhaa.
Rais huyo wa zamani wa ujerumani ambaye pia ni mtaalamu wa uchumi na mwanasiasa wa Christlich Demokratische Union(CDU) cha ujerumani, ameeleza kushangazwa kwake na haraka inayoonekana katika kuzifanya nchi za Afrika Mashariki kuwa na sarafu ya pamoja. Amesema kwamba jambo hilo ni nyeti na linahitaji muda mrefu zaidi wa wananchi wanchi hizo kushauriana na kujadiliana kabla ya uamuzi wa kuwanayo haujafikiwa.
“Kwa nini kuna haraka katika jambo la msingi na muhimu kama hili?alihoji
Proffesa Kholer anayasema haya wakati baadhi ya nchi wanachama wa E.U zikikabiliwa na matatizo makubwa kufuatia sarafu ya pamoja ya EURO nchi hizo ni kama Ugiriki,Spain na Ireland.
E.A.C(East African Community)
Kwa habari zaidi http://www.raiamwema.co.tz/rais-wa-zamani-ujerumani-ashangaa-uharaka-wa-sarafu-ya-pamoja-eac
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen