Best Blogger TipsSoon

Samstag, 18. Juni 2011

TZMPAKAAU

Spika wa bunge sasa ashtakiwa
  • Ni kwaajili ya upendeleo na upindishaji wa kanuni  kwa makusudi

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemshtaki Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwa kamati ya Kudumu ya Kanuni za Bunge, kwa madai kuwa anapindisha kwa makusudi kanuni za Bunge ili kuwakandamiza wapinzani na kuwapendelea mawaziri na wabunge wa CCM.

Spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda

Msimamo huo ulitaangazwa jana na Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), kwa waaandishi wa habari mjini Dodoma

Mbunge wa Singida Mashariki(CHADEMA) Tundu Lissu

Alisema Spika anazijua vyema akanuni za Bunge kwa kuwa amekaa bungeni kwa zaidi ya miaka 30 na amekuwa Naibu Spika kwa miaka mitano, lakini anapoona maslahi ya chama chake yanaguswa amekuwa kwa makusudi akipindisha kanuni kuwabana wapinzani.

Alitoa mfano jinsi Spika alivyokataa Waziri Mkuu asijibu swali lake katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo juzi, akidai kuwa suala hilo liko mahakamani na haliwezi kujadiliwa na Bunge kwani kufanya hivyo ni kuingilia mhimili mwingine wa mahakama.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mke wake bi Tunu Pinda

Lissu alimuuliza Pinda kama imekuwa sera ya serikali ya Tanzania kuua raia wake na wahusika kutochukuliwa hatua zozote kwani wananchi wanaozunguka mgodi wa North Mara wamekuwa wakiuawa na polisi na walinzi wa mgodi huo bila kuchukuliwa hatua.

“Spika alikataa swali langu lisijibiwe kwa madai kwamba suala hilo liko mahakamani na alipoombwa mwongozo wake kutokana na ukweli kwamba hakuna kesi hata moja ambayo imefunguliwa au inayoendelea katika mahakama yoyote ya Tanzania inayohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo au yanayowahusu polisi wanaohusika na mauajai hayo, Spika alidai kwamba wauliza maswali wenyewe walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya jinai katika mahakama ya wilaya ya Tarime yanayotokana na matukio ya mauaji ya watu watano yaliyofanywa na polisi kwenye mgodi huo,”alisema.


“Ukweli ni kwamba mimi sina kesi inayohusiana na mauaji ya Nyamongo, mimi na wenzangu tumeshtakiwa kwa kuingia kijinai katika eneo la kuhifadhia maiti hospitali ya wilaya ya Tarime, kufanya mkusanyiko haramu na kuwazuia mganga wa hospitali hiyo na askari polisi kufanya uchunguzi wa miili ya marehemu, sasa kesi hiyo inahusiana vipi na swali langu la mauaji ya Nyamongo kama sio kumkingia kifua Waziri Mkuu?” alihoji.
Alisema suala la mauaji ya Nyamongo halijawahi kufikishwa mahakamani hivyo kukataa swali lake lisijibiwe ni kuikinga serikali isiwajibike kwa makosa ya mauaji dhidi ya raia ambayo imekuwa kawaida.
Alisema inawezekana Spika alitoa msimamo huo bila kupewa maelezo sahihi kuhusu mauaji ya Nyamongo.



Spika wa sasa wa bunge  Anna Makinda

“Spika anakula kiapo cha kufanyakazi kwa kufuata kanuni na bila upendeleo, sasa na si mara ya kwanza anaonekana kwenda kinyume cha kiapo chake cha kufanya kazi bila upendeleo, kwa kuwa uamuzi wa Spika sio wa mwisho na kanuni zinaturuhusu kumshtaki tunampeleka kwenye kamati ili imchunguze na kutoa majibu ya suala hili haraka iwezekanavyo.

“Tulisita sana kuchukua uamuzi huu wa kumshtaki, lakini tumeona tukiacha mambo haya yataendelee na Spika atakuwa dikteta na mijadala muhimu itazimwa kila siku, barua ya malalamiko tumeshaikamilisha na leo tunaiwasilisha kwa kamati husika,”alisema Lissu.
Lissu alisema kwa kuwa malalamiko hayo yanamhusu mwenyekiti 

Vyanzo: TZMPAKAAU,Ippmedia.


Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen