Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 16. Juni 2011

TZMPAKAAU

Atakaye kalia kiti alichokiacha Osama  ni huyu
  •  Wamarekani waahidi kumkamata na kumuua
  •  Donge nono kutolewa kwa atakayesababisha kukamatwa kwake ni bilioni 37 za Tanzania(25million$)
  • Jamaa ni raia wa Egypt
  •  Baba na mama yake walikuwa madaktari
  • Yeye ana stashahada ya udaktari wa macho
Osama Bin Laden (left) and Ayman al-Zawahiri (file photo)
Kushoto ni aliyekuwa kiongozi wa Al Qaeda Osama na kulia ni Ayman Al zawahiri.
Ayman al-Zawahiri, ambaye kwa muda mrefu mno amekuwa msaidizi wa Osama Bin Laden katika kuiongoza Al-Qaeda, na akishikilia nafasi ya pili katika kutoa amri, sasa ataliongoza kundi hilo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa katika wavuti ya kundi hilo.
Ayman al-Zawahiri
Kiongozi mpya wa kundi la Al-Qaeda
Kundi la Al-Qaeda limeonya kwamba litaendelea na vita vyake dhidi ya Marekani na Israel chini ya uongozi wa Zawahiri.

Wadadisi wa masuala ya Al-Qaeda wanaelezea kwamba Zawahiri, mwenye umri wa miaka 59, na aliyezaliwa nchini Misri, ni mtu mwerevu sana, lakini hana uwezo wa kuwavutia wafuasi wengi kama alivyofanya Osama.

Baadhi ya wadadisi wanasema yeye ndiye aliyepanga na kuendesha shughuli nyingi zilizohusiana na shambulio la Marekani la 9/11.

Na haya ni maneno yake katika video aliyotolewa na Al Qaeda mwezi huu

"We must continue on [Bin Laden's] path of jihad to expel the invaders from the land of Muslims and to purify it from injustice.
The man who terrified America in his life will continue to terrify it after his death. You will continue to be troubled by his famous vow: You shall not dream of security until we enjoy it and until you depart the Muslims' lands.
America is not facing an individual or a group, but a rebelling nation, which has awoken from its sleep in a jihadist renaissance."

Source:BBC,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen