Best Blogger TipsSoon

Samstag, 11. Juni 2011

TZMPAKAAU

 Wabunge wa CHADEMA waamua
  • Kuanzia sasa hawataki posho
  • Wasema posho hizo zielekezwe kwingineko
  • Waeleza  iwapo posho hizo zitazuiliwa serikali itaokoa bilioni 900 za  walipa kodi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hoja ya kufuta posho za vikao kwa wabunge na watumishi wengine wa serikali ni hoja ya chama hicho na kwamba kwa kufanya hivyo fedha za walipakodi zaidi ya Sh. bilioni 900 zitaokolewa kwa mwaka.

Mbunge wa Hai kwa tiketi ya CHADEMA bw Freeman Mbowe

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge, muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kambi ya upinzani.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alisema mapendekezo hayo yatatolewa kama sehemu ya bajeti yao watakayoiwasilisha bungeni Jumatano ijayo.

“Hoja hii ichukuliwe kama hoja sensitive (muhimu), na isichukuliwe kama hoja ya kuleta migogoro miongoni mwa Zitto (Kabwe) na wabunge ama wabunge wa Chadema na wabunge wengine,” alisema Mbowe.

 Alisema wabunge na watumishi wengine wa serikali wamekuwa wakipata posho wakati wa vikao licha ya kwamba wamekuwa wakipata mshahara kila mwezi. Alitoa mfano wa mbunge ambapo amekuwa akipata posho ya kujikimu na vile vile akihudhuria bungeni anapewa posho wakati hiyo ni kazi ya mbunge.
Mbunge wa kigoma kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA

Hii inafuatia kauli ya Zitto Kabwe wiki iliyopita kuhusu ufutwaji wa posho za wabunge na utekelezaji wake ambapo yeye Zitto Kabwe alimuandikia  katibu wa bunge barua rasmi akitaka kufutwa kwa posho yake na iwekwe kwenye mfuko wa maendeleo ya Jimbo.

Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen