Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 9. Juni 2011

TZMPAKAAU

Mkulo na bajeti ya 2011/12

  • Vipaumbele vitano vya bajeti vyatajwa
  • Adai ni bajeti ya "common man" 

Mustapha Mkulo na briefcase yenye makadirio ya bajeti mwaka wa serikali  2011/12

Serikali imetangaza vipaumbele vitano vya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2011/12. Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alitangaza vipaumbele hivyo jana ambavyo ni nishati ya umeme, usalama wa chakula, miundombinu, ukosefu wa ajira na kudhibiti mfumuko wa bei.




Akielezea hali ya uchumi wa nchi amesema mfumko wa bei ulipanda mpaka asilimia 8.6 ikilinganishwa na mwaka uliopita wa bajeti.


Zaidi ya hapo amesema kwamba shilingi ya Tanzania imeendelea kushuka thamani kwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na mwaka uliopita.Hali hii inaiacha shilingi ya tanzania hoi ikilinganishwa na sarafu za kigeni kama dola na euro.


Mkulo alikuwa na taarifa njema pia, akieleza kukua kwa pato la taifa kutoka asilimia 6.0 mpaka 9.0 katika mwaka huu wa serikali.Na zaidi ya hapo alisema akiba ya fedha za kigeni imeendelea kukua hadi kufikia dola za marekani milioni 3948,kutoka dola milioni 3552 mwaka uliopita.


Vyanzo:Ippmedia,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen