Best Blogger TipsSoon

Samstag, 11. Juni 2011

TZMPAKAAU

  Syria hali inazidi kuwa tete
  
  • Sasa wanajeshi washambulia vijiji
  • Wachunguzi wa mambo wanadai ni kulipa kisasi  cha mauaji ya wanajeshi 120
  • Wakimbizi wa Syria wazidi kumiminika Uturuki


Clear message from Syrian protesters

Mwananchi mmoja wa Syria aliyeshuhudia baadhi ya matukio ya usiku wa Ijumaa, kaskazini magharibi mwa nchi, anasema wanajeshi wa Syria walitumia vifaru kushambulia kijiji karibu na mji wa Jisr al-Shughour.

Mtu huyo ambaye amekimbilia Uturuki, anasema jeshi liliangamiza mazao ya kijiji.

Shahidi huyo anaeleza kuwa shambulio lilianza alfajiri kabla ya watu kuamka.

Kijiji chake kiko kilomita nne nje ya Jisr al-Shughour, na kiko juu ya kilima.

Aliona shambulio dhidi ya kijiji kilioko chini ya kijiji chake, ambacho anasema, kiliingiliwa na vifaru 40.
Kilizungukwa na wanajeshi waliokuwa na bunduki, na vifaru vilishambulia nyumba, lakini hajui watu wangapi walikufa.

Shahidi huyo anasema aliona kijiji chake nacho kitakutwa na hatima hiyo hiyo, na aliamua kukimbilia Uturuki pamoja na mkewe, watoto 10 na farasi wake wane.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen