Best Blogger TipsSoon

Dienstag, 7. Juni 2011

TZMPAKAAU

Majibu kwa kauli ya Madaraka Nyerere
  • Ni kuhusu ujenzi wa barabara itakayopita Serengeti


Kujenga barabara katika mbuga ya wanyama Serengeti ni jaribio la kutengeneza new ecosystem (ecological system) lakini swali kubwa ni je unapojaribu kutegeneza ecosystem yako umefanya utafiti wa kutosha kwamba haina madhara kwa viumbe waliokuwepo au viumbe waliokuwepo wataipokeaje?

Lakini pia ikumbukwe kwamba kujenga barabara eneo la mbuga itapelekea uchafuzi wa hewa kutokana na gesi zitokanazo na magari n.k,achilia mbali hilo kutakuwa na sound pollution kwani engine za magari yetu tunazijua ni kama magenerator yanayotembea kama tungekuwa na electric cars(magari ya umeme )hili lisingekuwa tatizo,lakini bado kuna uchafuzi wa watu ambao watatupa taka zinazoweza kuathiri wanyama kwa njia moja au nyengine kama sio kupelekea kufa kwa wanyama hao.

Air pollution which may be cause by only one car at a point

Kingine ambacho naweza kumkumbusha kaka madaraka ni kwamba je anasahau kwamba ujenzi wa barabara  katika mbuga hii ni kama uwezeshaji majangili ujenzi wa barabara utaongeza uwindaji haramu mara dufu lakini kama kweli kuna nia ya kuwaletea majangili neema basi hili lifanyike lakini vinginevyo kuna kilasababu ya kulaani ujenzi wa barabara hii.


A dog performing his tasks at home


Dolphins could be intelligent than some people

  • the size of brain is an indication of intelligence some of the dolphins have bigger brain than human brain
  • they do have the talent in solving problems
  • they can communicate
  • sometimes dolphins invet and play complex games
Embu tujifunze kutoka kwa wenzetu watu wa magharibi a.k.a wazungu wao walikuwa na wanyama kama sisi zamani lakini kutokana na urbanization and modernization wakajenga barabara,nyumba na vinginevyo mpaka maeneo ya wanyama leo hii wamepoteza wanyama wote na sasa wanalitoa mabilioni ya dola ili  kwa njia yeyote ile ili waweze kuona  wanyama hao .Wahenga walisema "kipya kinyemi ingawa kidonda",jamani tuache huu mtazamo wa kila kitu kipya ni kizuri.....


Lakini hapa kuna dhana nyengine ambayo nahisi ipo kwamba wengi wetu tunaona kwamba wanyama na viumbe wengine ni vikwazo kwetu na hii inawezekana kuwa ukweli kwa upande mmoja,lakini upande mwingine wanyama hawa wanafaida nyingi saana saana kwetu ....mfano wanasayansi sasa wanahofia kupotea kwa wadudu kama nyuki na jamii yake ambao kwa kiasi kikubwa wanachangia uzalishaji wa mimea na wanasayansi wanasema iwapo wadudu hawa wakitoweka dunia itatumia mabilioni ya dola ili kuwezesha uzalishaji wa mimea,ukiachana na hilo mbwa ambao wengi wetu tunawaona kama maadui mbwa hawa wanaweza kutumika kutambua madawa ya kulevya,kutambua magonjwa kama kifua kikuu na kama usafiri maeneo ya baridi.Sisi tunapo mchukia mjusi ,mjusi ambaye mungu wangu hana tatizo na mtu yeyote ,wenzetu wanamsoma na kuangalia uwezo wake wa kupanda hata kwenye dari na kutembea bila tatizo ili waweze kuutumia ujuzi huu kwa mambo mengine.
Sasa leo tunaona simba,chui,punda milia,tembo na wengineo waliopo Serengeti kama wanazuia riziki zetu kwa njia moja au nyengine watakapotoweka ndio tutajua kumbe wao ndio walikuwa riziki yenyewe
Tuache maneno ya kisiasa ......

Source :MICHUZI,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen