Best Blogger TipsSoon

Freitag, 3. Juni 2011

TZMPAKAAU

  Je unamfahamu GILA MONSTER?
  • Anatajwa kama mjusi mwenye sumu zaidi

  • Gilla ni kwasababu walikuwa wakipatikana kwa wingi katika mto Gilla Arizona marekani


Basi huyu ni mjusi anayeitwa Gilla Monster kwa jina la kitaalamu anaitwa Heloderma suspectum

Maeneo anayopatikana
Gila monster anapatikana sana kusini magharibi ya U.S.A na Mexico.Mara nyingi Gilla monster anapatikana maeneo yenye vichaka ya jangwani na chini ya mawe jangwani.Majimbo anayoweza kupatikana huko marekani ni kama Utah,New mexico,Nevada,Carlifonia na Arizona.Siri ni moja Gilla Monster ni mjusi anayependa sana majimaji au unyevu lakini anaishi jangwani



Ukubwa wake
Gilla lizard mkubwa kabisa huweza kufikia ukubwa wa futi 2 sawa na sentimeta 60.Na ki Gilla Monster  kilichotoka kuanguliwa huwa na sentimeta 16.3 hivi lakini kijusi hiki  kinaweza kuuma pia.


Chakula chake
Chakula kikuu cha gila monster ni ndege na mayai ya reptilia wengine lakini gila monster hula wadudu,chura na mamalia wengine kama panya n.k.





Gilla Monster hula mara chache sana kama hayupo kwenye zoo,inakadiriwa Gilla Monster hula kati ya mara tano au kumi kwa mwaka mzima siri watch the video

Gilla monster huliallocate windo lake kwa kutumia harufu, anaweza kunusa hata yai lililofukiwa sentimeta 15 chini ya ardhi


Tabia
Asilimia 95% ya maisha yake gilla monster huishi chini ya ardhi,na asilimia nyingine 5% hutumia kuota jua,kutafuta chakula n.k

Gilla Monsters hutaga mayai yao kati ya July na August na huyafukia sentimeta 13 chini ya ardhi na kipindi cha kuatamia ni kama kwa binadamu miezi tisa.

As all creatures Male gilla monsters they do often fight for females and territories style of fighting is wrestlling style


Hatari yake

Mjusi huyu huuma na akiuma anatema Venom na venom ni neurotoxin ambayo ni SUMU . Wanasema muathirika hupata maumivu makali sana pale anapokung'ata kwa taarifa zaidi watch video,lakini uzuri wake huwa hana speed kabisa

Jinsi ya kumsaidia mtu aliyeng'atwa
Kama bado mjusi yupo basi mzamishe kabisa ndani ya maji ili aachilie sehemu anayouma.Na baadaye ni muhimu kwenda hospitali kwani huwa anasumu kali kiasi

Utafiti
Shirika la usimamizi wa dawa na chakula la marekani mwaka 2005 liliidhibitisha na kisha kuruhusu dawa iitwayo Byetta kwa ajili ya kutibu type 2 diabetes (kisukari)dawa hii ilitengenezwa kwa kutumia aina fulani ya proteini inayopatikana katika mate ya mjusi huyu....na miaka mitatu baadaye ya utafiti ikaonesha kweli watu wenye type 2 diabetes wamesaidika na sasa hivi kunatafiti mbali mbali zinaendelea juu ya mate ya mjusi huyu

       Videos related to Gilla Monster
                                              Ana kwa ana na Gilla Monster




Gilla Monsters Bite


So always have fun,be nice ,learn new stuffs if chances are there,stay safe  respect Gilla Monsters.

Vyanzo:TZMPAKAAU,Wikipedia,Helium.com,Youtube:Gilla Monster Encounter and Gilla Monster bite,painful and dangerous.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen