Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 2. Juni 2011

TZMPAKAAU

   DAH MUNGU MKUBWA
  • Ilikuwa mitaa ya saa nne usiku 01.06.11
  • Ajali live ya daladala Mandela road
  • Hii ndiyo daladala yenyewe ikiwa mtaroni
    Wasamaria wema wakijaribu kuwasaidia jamaa wawili walionasa ndani ya daladala hiyo
    Wasamaria wema wakaita crane ili inyanyue daladala, na kurahisisha kazi ya kuwaokoa watu waliokuwa wamenasa 
    Wasamaria wema wakifanya juhudi kubwa kabisa kuwasaidia ndugu zao walionasa ndani ya gari,
    wasamaria wema walikuwa sharp na walijaribu kila lililowezekana kuokoa.
    Jamaa aliyenasa ndani ya daladala hilo akiangalia hatima yake.
    Juhudi za uokoaji zilizaa matunda baada ya jamaa wote wawili kuokolewa wakiwa salama salimini,bila majeraha yaliyoweza kuonekana.
    Hapa askari akiomba msaada kwa mpita njia, ili asaidie kubeba jamaa waliopata ajali kuwapeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi. Mama alionesha pingamizi dogo akidai muda ulikuwa umekwenda sana na angependa kuwahi nyumbani.
    Wakati mpita njia huyo akiendelea  na pingamizi lake, wasamaria wema walikuwa wameshawapakiza wateja wao na kwa staili hii walikamilisha zoezi zima la uokoaji.
    Nichukue nafasi hii kuwapongeza wasamaria wema wote waliowaokoa ndugu zetu yaani walifanya kazi nzuri kama proffesionals na kwa moyo safi BIG UP!!!

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen