Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 2. Juni 2011

TZMPAKAAU

Jamii ya watu wachina waishio Tanzania waonesha mfano



Jumuiya ya watu wa China waishio nchini, wamewapatia misaada yenye thamani ya Sh. milioni 5 watoto yatima waishio katika kituo cha Kurasini jijini Dar es Salaam.



Akikabidhi msaada huo jana kituoni hapo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Bai Lingbo, alisema katika maadhimisho ya siku ya mtoto duniani ambayo hufanyika kuanzia Juni 1 kila mwaka wameona ni vyema kuwajali watoto hao kwa kuwapatia zawadi mbalimbali ili wajisikie bado wako na familia zao.

"Tumeamua kuwapatia watoto hawa zawadi hizi ili nao wajione kama hatujawasahau na bado tunawajali na kushiriki nao katika michezo mbalimbali ambayo itawafanya wafurahi zaidi," alisema Lingbo.
Lingbo aliitaja misaada waliyoitoa katika mashirika mbalimbali kutoka kwenye jumuiya huyo kuwa ni vifaa vya kuchezea vya watoto na mipira, nguo, dawa za kuzuia malaria, vifaa vya shule,pea 120 za kandambili,masanduku ya kuhifadhia nguo 50 na mikate na biskuti.


Bi Bai Ling Bo akimkabidhi msaada huo bi Magreth Mkandawile ambaye ni msimamizi wa kituo hicho

Aidha, mlezi wa kituo hicho Magreth Mkandawile,aliishukuru Jumuiya huyo na kusema kuwa ni mara ya pili kupeleka misaada katika kituo hicho kwani mara ya kwanza walipeleka fedha taslimu milioni mbili na ziliwezesha kuwalipia ada watoto hao.
"Tunawashukuru sana kwa moyo wao wakujitolea kwani mwanzoni mwa mwaka huu walitoa fedha ambazo zimesaidia kuwalipia karo wanafunzi wa sekondari na walituahidi kuwa ule ulikuwa ni mwanzo na kweli leo tunaamini kutokana na misaada waliyoleta," alisema Mkandawile.
Pia aliwaomba wafadhili wanaokwenda kutoa misaada na kuwachukua baadhi ya watoto hao na kwenda nao nyumbani kwao waendelee na moyo huo kwani hiyo inawafanya watoto hao kupoteza mawazo ya ukiwa na kujiona kuwa kuna watu wanaowajali.

Vyanzo:Ippmedia,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen