Best Blogger TipsSoon

Samstag, 28. Mai 2011

TZMPAKAAU

Mazuri  yao tuyaige  , mabaya  yao tusiyafuate

Wachina  wengi  wanaishi  kwa msemo huu"Mazuri yao tuyaige...". Na  hii ni  siri  kubwa sana katika mafanikio ya Watu wa jamhuri ya uchina na majirani zao.  Kama uthibitisho

Kijana huyu wa kichina ambaye ni kinyozi na mwanamitindo ya nywele ameanza kutengeneza gari yake aina ya Lamborghini  Reventon.Kijana Asan kutoka mji wa Kunming  jimbo la Yunan nchini China anasema  Lamborghini  Reventon   ni gari nzuri lakini bei yake ipo juu sana hivyo ameamua kuiga mtindo wa gari hiyo na kutengeneza   Lamborghini   yake mwenyewe,kutumia gari yake ya mwaka 1995  aina ya  Nissan CefiroA31.Anakadiria atatumia dola 14,000 tu kukamilisha ndoto yake .



Hii ni  Lamborghini  Reventon halisi .

replica of the new Lamborghini Aventador 002 A Chinese man has made replica of the new Lamborghini Aventador

Huyu ndo jamaa anakomaa kukamilisha ishu yake



Lamborghini Reventon  halisi  ikiwa imefunguliwa milango yake

replica of the new Lamborghini Aventador
Kijana Asan  anasema milango sio kazi labda waseme kingine

Kama hiyo haitoshi kuna kundi moja la Orchesta la watu wa jamhuri ya uchina wameweza kuuimba vizuri kabisa mwimbo wa Malaika, wimbo ambao umepata umaarufu mkubwa na kuimbwa na kurekodiwa mara kwa mara na wanamuziki mbalimbali ikiwajumuisha Boney M.




sasa   swali ni je wewe unaiga mazuri ya wenzako  au...?


Vyanzo:TZMPAKAAU,Wikipedia,Toried

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen