Best Blogger TipsSoon

Dienstag, 24. Mai 2011

TZMPAKAAU

    

MADAI  YA   WAZEE WA AFRIKA MASHARIKI YATUPILIWA MBALI


 Kwa niaba ya wazee wenzake, Mohamed Matibwa (84) alisema kuwa wamesikitika na kitendo cha mahakama kuwaambia kuwa hawana haki katika madai yao.Wazee hao walikuwa wakishinikiza kupatiwa madai yao ya mafao ya Jumuiya hiyo iliyovunjika mwaka 1977.Hukumu ya kesi hiyo ilimalizika saa 6:00 ,Huku mahakama ikibatilisha madai ya wazee hao waliosota kwa muda mrefu kutafuta haki yao.

Wazee wa afrika mashariki walipoenda ikulu kudai chao

Kama kuonesha kutoridhishwa na hukumu hiyo ya mahakama Kuu wazee hao wanyonge walilala barabarani na kusema litakalotokea na litokee,hivyo kuifanya barabara ya posta kivukoni isipitike mbali ya hayo wazee wengine walionekana wakiwa katika hali ya majonzi na wengine walisikika wakisoma dua mbaya kwa viongozi wa serikali.


"Basi bora nife" kama anavyoonekana mzee mmojawapo

Ikumbukwe tu kwamba wazee hawa walilitumikia taifa kwa nguvu akili na uwezo wao kupitia jumuiya ya afrika mashariki kati ya mwaka 1967 mpaka jumuiya hiyo ilipovunjika katika mwaka wa 1977.Kwaiyo wazee hawa wamezungushwa na serikali yao kwa miaka zaidi ya 34 na mwisho wa uzungushaji huo ulikuwa jana.

Na ili kuweka kumbukumbu vizuri ,Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipovunjika  serikali ya Uingereza iliunda tume na baadaye kutoa malipo ya mafao kwa wafanyakazi wote wa jumuiya  katika rate ya paund kuhofia kupanda na kushuka kwa thamani ya hela za Tanzania, Uganda na Kenya. Serikali za Kenya na Uganda  zilikwishawalipa wafanyakazi wake  wote wa jumuiya hiyo malipo halali, ila serikali ya Bongo hadi jana ilikuwa haijawalipa wafanyakazi wake.

Wazee hawa  wameshatumia muda mwingi(toka mwaka 1997) ili kufuatilia madai yao na zaidi ya hayo wazee hawa wametumia pesa nyingi kuwalipa mawakili wao ili kutetea haki yao dhidi ya serikali .Lakini ndo ivyo ...

Mzee mstaafu wa jumuiya ya afrika mashariki akiwa haelewi nini cha kufanya baada ya hukumu hiyo


















Wazee hao,waandishi wa habari na wananchi wengine wakiwaombea viongozi wa serikali na serikali inaowanyayasa na kuwanyima haki yao kila la kheri

Vyanzo:TZMPAKAAU,LUKAZA,IPPMEDIA,youtube Dk.Slaa

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen