Best Blogger TipsSoon

Montag, 23. Mai 2011

TZMPAKAAU

  Je wajua ?
   Peregrine Falcon ndiye kiumbe mwenye mwendo kuliko wote duniani....




Peregrine Falcon  ana uwezo wa kwenda zaidi ya  mile 200 kwa lisaa ambayo ni zaidi ya 320 km/h hii inamfanya kuwa kiumbe mwenye mwendo kasi mkubwa zaidi kuliko yeyote yule duniani.

Ndege ndilo windo penzi la  Peregrine Falcon   na ili kulipata basi Falcon anahitaji mwendo wa mshale. Kutokana na mwendo huu Falcon mara nyingi  hulikamata windo lake likiwa bado angani.

Mara chache Ndege huyu hula reptilia kama mijusi na nyoka au mamalia kama panya na sungura.



Peregrine Falcon akiwa kazini

Peregrine Falcon huwa na urefu wa kati ya sentimeta 34 -58 na upana wa mabawa kati ya sentimeta 80 -120.Ndege huyu huweza kuishi mpaka miaka 15.5

Tabia nyengine za kuvutia
Peregrine Falcon akifikisha miaka miwili  2 au 3 hupata mwenzi wa maisha "Pair mate for life" na wawili hawa  watabakia pamoja maisha yote mpaka mmoja atakapo kufa .

 Ratiba ya uzazi 
 Peregrine Falcon   kila mwaka mara moja "Pair mate for life"huatamia na kuangua vifaranga wapya kipindi gani cha mwaka hii hutegemea eneo ambalo ndege hawa wapo lakini in North Hemisphere ni ndege hutaga,kuatamia na kuangua mayai yao kati ya mwezi Februari na Machi na in South Hemispere ni kati ya mwezi  Julai na mwezi Juni.

 angalia hizi video  kuona kama kuna BMW au Benz inayoweza kumshinda kwa mwendokasi





Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen