Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 11. Mai 2011

TZMPAKAAU

  Magufuli aahidi kuwasha moto
  • Moto kuwababua wote walioweka mabango kwenye hifadhi za barabara
  • Asema hakuna atakayeweza kuuzima

Hapa Magufuli akipata kikombe cha babu kwanza ili kujiweka fiti   ...."si unajua kazi na dawa"

Licha ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuacha ubabe. Waziri huyo amepania kwa vyovyote iwavyo ni lazima abomoe mabango yote ya biashara ya barabarani.

Magufuli alianza kukoleza  moto huo jana, safari hii akisema hakuna wa kumzuia kuondoa mabango hayo kwa kuwa anatekeleza sheria za nchi.

Alisema kuanzia sasa wenye mabango wasipoyaondoa kwa hiyari yao, yeye atayaondoa kwa nyundo.


Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli

Akizungumza jana kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV, Dk. Magufuli alisema hakuna wa kumzuia kutekeleza wajibu huo kwa sababu anachokifanya ni kufuata sheria inayolinda barabara.

Waziri Magufuli alipinga utetezi uliotolewa hivi karibuni na kiongozi mmoja wa Halmashauri (hakumtaja) kuwa mabango hayo yanaongeza kipato kwa kukusanya kodi.

Alisema hakuna ushahidi wa jambo hilo kwani fedha zinazokusanywa zimekuwa zikiishia mikononi mwa watu binafsi na wala serikali hainufaiki na chochote.

“Mkakati wangu utabaki palepale hauwezi kubadilika, ni lazima mabango yataondolewa ili kuweka barabara zetu salama na safi, haiwezekani barabara zijengwe kwa mabilioni ya pesa halafu mtu anakuja kuharibu kwa kuweka mabango,” alisema Dk. Magufuli.

Hivi karibuni Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alikaririwa akipinga hatua hiyo kwa kueleza Halmashauri yake inapata mapato mengi kutoka kwenye mabango hayo ya biashara, fedha ambazo zinatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Lakini Pombe Magufuli alikanusha kauli hiyo kwa kusema  “Hakuna pesa za mabango zilizojenga barabara, kama zipo watuonyeshe basi  tuone kuliko kueleza tu kwa maneno, hizi pesa wanajilipa posho tu, " alisema.

Kama kuonesha msisitizo wake katika hili waziri alisema   "Kimya kingi kina mshindo na hivi karibuni mtaona mambo yangu".

Source :NIPASHE,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen