Best Blogger TipsSoon

Samstag, 2. April 2011

TZMPAKAAU

 Dirndl und Leder hose
Dirndl na Leder hose ni nguo za kitamaduni hapa Austria.Dirndl ni kijigauni cha kitamaduni mahususi kwa wanawake na Leder hose ni suruali au bukta mahususi kwa ajili ya wanaume.Mavazi haya yanahistoria ndefu sana kwa wa Austria na bado hayajapoteza umuhimu wake.Juzi kulikuwa na party iliyoenda kwa jina la Dirndl na Leder hose party katika chuo kikuu cha Hagenberg na ndo maana nimeona nishare na wadau juu ya mavazi haya.

 Sio nyumbani tu utamaduni ni muhimu  ni kila mahali  ni  dirndl kwenda mbele,afu   kama unavyoona dirndl hizo zinatofautiana kwa rangi na mishono.


Hawa wadau wengine saana wengine wakiwa wamepozi ndani ya dirndl na leder hose,
     asa waliniuliza mara kadhaa wewe leder hose yako ipo wapi? Nikasema nyumbani kwetu hatuna leder hose tunatumia majani au magome ya miti kama mavazi ya asili.
Hii ni picha ya miss na mister leder hose.Sasa haya ni mavazi ya enzi na enzi hapa Austria lakini wataalamu wa mitindo huwa wanayamodify kila kipindi ili yaweze kwenda na wakati lakini pia yasipoteze ile ladha yake ya asili.Ila siri ni kwamba kama leder hose inauzwa si chini ya laki nane za kibongo na dirndl si chini ya laki tatu za kibongo.
Leder hose, kama inavyoonekana hapo juu hutengenewa kwa ngozi ya paa na leder hose yenye thamani kubwa kabisa hushonwa kwa mikono tu bila mashine.

Asa zamani karne kadhaa zilizopita kwa wa Austria dirndl na leder hose  ilikuwa ndiyo vazi la kila siku na  vazi la  sherehe vilevile,  dirndl na leder hose   za sherehe zilikuwa zimenakshiwa zaidi.Na zamani kila eneo lilikuwa na dirndl na leder hose ya aina yake. Kwa msingi huu kama wangejumuika katika tukio fulani walitambua kupitia aina ya mavazi haya  kuwa huyu katoka wapi na huyu katoka wapi.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen