Best Blogger TipsSoon

Sonntag, 3. April 2011

TZMPAKAAU

Mbunge ajitolea magari ya wagonjwa

Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahmmoud H. Mgimwa.

Mbunge huyo ametangaza kuwa atazitumia  shilingi milioni 90 alizopewa na Serikali kwa ajili kjiununulia gari,  kununua magari matatu ya kubebea wagonjwa katika jimbo lake.
Akizungumza katika Mkutano uliowajumuisha wananchi wa Mufindi wanaoishi jijini Dar es Salaam jana, Mgimwa alisema fedha walizopewa na serikali kwa ajili ya kununulia gari la kifahari, atazijumuisha na fedha alizopewa na wafadhili wengine ili kununua magari matatu yatakayowasaidia wananchi wa tarafa tatu zinazounda jimbo hilo.
Alisema magari hayo yatatumiwa kwa ajili ya kubebea akina mama wajawazito wakati wa kwenda kujifungua pamoja na wagonjwa mahututi wanaotakiwa kuwahishwa hospitalini yatakabidhiwa hivi karibuni yakitokea Dubai.Mwisho aliwataka wanamufindi wanaoishi maeneo mbalimbali kuchangia  katika maendeleo ya  jimbo lao.
Alitaja tarafa zitakazokabidhiwa magari hayo kuwa ni Sadani, Ifwaji na Kibengu.
Vyanzo:Nipashe,TZMPAKAAU. 

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen