Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 27. April 2011

TZMPAKAAU

SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Rais Kikwete na Jenerali Davis Mwamnyange


Rais wa Muungano Kikwete akiligagua gwaride katika maadhimisho ya
miaka 47 ya muungano



Rais akimsalimia mjane wa muasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar mke wa Karume
Fatma Karume


Rais wa Muungano akisalimiana na rais wa sasa wa Zanzibar DK.Ali Mohamed Shein

Licha ya mvua kubwa kunyesha jana, Watanzania wameadhimisha miaka 47 ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Maelfu ya wananchi walianza kujitokeza mapema mara baada ya kuswali alfajiri, kuelekea katika uwanja wa Amaan ambapo milango ilianza kufunguliwa kuanzia saa moja asubuhi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliwasili katika uwanja huo majira ya saa nne asubuhi akiwa katika gari la wazi, ambapo aliambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange.

Vikosi  vya Ulinzi na usalama, vilitoa burudani tofauti, ikiwemo kujipanga na kujenga umbile lenye kuonesha alama ya miaka 47 ya Muungano na kutengeneza herufi za ufupi wa Tanganyika TNG na ZNZ.

Vijana 700 wa halaiki kutoka shule mbalimbali za Tanzania bara na Zanzibar, nao walikuwa sehemu ya burudani katika maadhimisho hayo, kutokana na michezo mbalimbali waliyoionesha ikiwa imebeba ujumbe wa kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Vijana hao walionesha burudani hiyo, kwa muda mrefu licha ya kunyeshewa na mvua kubwa ambayo ilisababisha ratiba ya maadhimisho hayo kufupishwa ikiwemo vikundi vya ngoma kukosa nafasi ya kutumbuiza.

Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, uwanja wa Amaan ulipambwa kwa picha za waasisi wa muungano Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Marehemu Abeid Amani Karume pamoja na picha za Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

Vyanzo:Ippmedia,Michuzi Blog,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen