Best Blogger TipsSoon

Samstag, 16. April 2011

TZMPAKAAU



Wanigeria Wapiga kura Leo

Wanigeria leo tar 16.04.2010 wanapiga kura ya  kumchagua rais wa nchi hiyo.

Nigeria ambayo ni nchi yenye idadi kubwa ya  watu kuliko nchi yoyote barani afrika, leo itawapigia kura watu wanne tu kwa ajili ya nafasi hiyo.

Mpiga kura mmojawapo huko nigeria kama alivyonaswa na kamera
Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha People's Democratic (PDP) anachuana vikali na Meja Jenerali Mstaafu Muhammadu Buhari wa Congress for Progressive Change (CPC), Nuhu Ribadu wa Action Congress of Nigeria (ACN) na Ibrahim Shekarau wa All Nigeria People's Party (ANPP).


Rais wa sasa wa Nigeria Goodluck Jonathan ambaye anakitetea kiti chake leo
Buhari na Ribadu wanaonekana kutoa upinzani mkali kwa Rais Jonathan, lakini huenda rais huyo akashinda kwa kiwango kidogo. Buhari aliwahi kuwa rais aliyeingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi hapo mwaka 1983 kabla naye kupinduliwa na Jenerali Ibrahim Babangida miaka miwili baadaye.

Ribadu ndiye mgombea kijana kabisa akiwa amezaliwa mwaka 1960, na ndiye aliyekuwa mkuu wa kamisheni ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria, ambayo ilichukua hatua kali dhidi ya mafisadi nchini humo baina ya mwaka 2005 na 2006.

Uchaguzi wa leo unatarajiwa kurejea mafanikio ya uchaguzi wa bunge wa wiki iliyopita, ambao pamoja na matukio ya hapa na pale, umetajwa kuwa ulikuwa mzuri zaidi kulinganisha na chaguzi zilizopita kwenye nchi hiyo.
Vyanzo: Deutsch welle,TZMPAKAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen