Best Blogger TipsSoon

Samstag, 16. April 2011

TZMPAKAAU

Kanisa la Mariendom Linz   Mariendom Cathedral in Linz

Basi kama unavyoona ni ndani ya kanisa la Mariendom

Marien dom  ni kanisa lililojengwa kwa miaka 62.....na lilifunguliwa rasmi mwaka 1924baada ya kukamilika

Lina viti 20,000.

Lipo Linz Austria

Ndilo kanisa kubwa kuliko yote hapa Austria.

 Lakini sio kanisa refu kuliko yote Austria  lina urefu wa meta 135 likiwa fupi kwa meta 2 tu kuliko kanisa refu kuliko yote hapa Austria.

Kwa nini Marien dom sio kanisa refu kuliko yote Austria?

 kipindi cha ujenzi wa kanisa hili Austria ikiwa Austria Hungary kulikuwa na sheria inayopinga jengo lolote lile kuwa refu kuliko kanisa kuu  katoliki la Vienna Stephen's dom.

Na ni kutokana na sheria za kipindi hicho majengo mengi ya  Austria huwa mafupi kuliko mnara wa kanisa refu zaidi katika eneo husika.

Kanisa  liliharibiwa kidogo upande wake wa kusini kipindi cha vita ya pili ya dunia na hali hii ilisababisha madirisha yake ya upande huu kubadilishwa na kuwekwa madirisha ya kisasa .


Upande wa kaskazini wa kanisa la Mariendom angalia hawa jamaa walivyokuwa wachapakazi
yaani utajiuliza hiyo mitofali waliifikishaje huko juu bila kuwa na cranes.Au hizo nakshi nakshi walizoweka utajiuliza walienda vyuo gani vya sanaa na walipata wapi vijifaa.





 Watalii wengi hupendelea saana kutembelea hili kanisa hasa summer ili kujionea ustadi wa wajenzi wa zamani.






Hii ni saa ya misa kanisa linauwezo wa kuchukuwa watu 20,000 wote wakiwa wamekaa. Na kuna heating system nzuri sana kipindi cha baridi mpaka kwenye seats lakini ni watu wangapi unaojionea.Inasikitisha jamaa wa hawana muda wa sir God.


Basi kanisa pia lina hoteli ya kisasa saana ni kwa ajili ya wageni wote wa kanisa na watalii kutoka maeneo mbali mbali duniani wanaofika   ili   kujionea kanisa.

Chanzo:TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen