Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 31. März 2011

TZMPAKAAU

Proffesa Safari ajiunga na chadema

Aliyekuwa mwanachama maarufu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Abdalah Safari, amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukimwagia sifa kuwa hakina udini wala ubaguzi.

Proffesa Safari akikabidhiwa kadi ya uanachama na mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe

Alisema safari yake ya kujiunga na chama hicho imechukua muda wa miezi mitatu ya majadiliano kwa kuwa baada ya kutoka CUF ambako alipata misukosuko mingi, familia yake ilimshauri apumzike.
“Baada ya misukosuko ya CUF familia yangu iliogopa sana mimi kurudi tena kwenye siasa, mke wangu na watoto walinishauri nitulie na niendelee na kufanyakazi ya kutunga vitabu tu, mke wangu hakutaka kabisa nirudi kwenye siasa, lakini nimekaa nao na tumefikia mwafaka ndo maana leo hii niko Chadema,” alisema jana.Wadadisi wa mambo wanasema inawezekana chadema ikamsimamisha Proffesa safari kama mgombea urais mwaka 2015. kwa habari zaidi tembelea http://www.ippmedia.com/.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Nipashe na Vijimambo

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen