Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 30. März 2011

TZMPAKAAU

PINDA:India inakaribishwa Tanzania
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda, amesema India inaweza ikawekeza katika  utalii, madini na kilimo nchini  Tanzania  kuisaidia nchi kuendeleza uchumi kwa haraka na kupambana na umasikini.
Pinda alikuwa akizungumza na ujumbe wa waandishi wa habari waandamizi  ulioko katika  ziara fupi nchini Tanzania jijini Dar es Salam jana.
Alisema katika utalii, wawekezaji kutoka India wanaweza wakawekeza katika biashara ya mahoteli na miundominu mingine ya kuiendeleza sekta hiyo ambayo ina nafasi nzuri ya kukuza uchumi.
Alisema Tanzania ina madini ya uranium, chuma na makaa ya mawe na ni eneo jingine zuri la kuwekeza.
Kuhusu Kilimo, Pinda alisema Tanzania ina hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo na ni robo tu ya eneo hilo ndiyo linalolimwa na hivyo kuna nafasi nzuri ya uwekezaji.
Waandishi hao kutoka katika magazeti makubwa ya india, walimuuliza Waziri Mkuu kuwa kwa jinsi hali ilivyo, Bara la Afrika linagombaniwa tena kama vile ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
CHANZO: NIPASHE

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen