Best Blogger TipsSoon

Samstag, 26. Februar 2011

TZMPAKAAU

Wataalamu :Miradi mingi haifanyiwi tathmini ya mazingira

Picha ya coco beach kutokea sea cliff

Imeelezwa kuwa miradi mingi inayowekezwa hapa nchini, haifanyiwi tathmini ya kimazingira (EIA) na hivyo kuwa hatari katika harakati za utunzaji wa mazingira.
Kauli hiyo ilitolewa jana katika semina iliyowahusisha wataalamu wa mazingira iliyoandaliwa na Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) na wataalamu mbalimbali.
Wataalamu hao walisema kuwa kwa sasa kinachofanyika katika baadhi ya majengo mengi nchini, ni kujengwa bila kushirikishwa kwa wataalamu hao na badala yake hutokea uharibifu wa mazingira.
“Tunaomba NEMC iwe makini kwa hili, kwani kwa sasa utakuta jengo limeibuka na ukiangalia halijafanyiwa tathmini na mtaalamu wa mazingira, na athari zake hutokea baadaye, NEMC iwabane watu hawa kwani bila kufanya hivyo tatizo hili halitoweza kuisha, kwani tatizo hili limekithiri kwa kiasi kikubwa mijini, mbali ya mikoani," alisema mtaalamu mmoja.
Naye mkuu wa Mazingira wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Sanjo Mgeta, alisema taasisi yake kabla ya kutoa mkataba wa ujenzi wa barabara kwa mkandarasi yeyote inahakikisha wanaweka tathmini ya mazingira jinsi itakavyokuwa katika ujenzi wa barabara husika.
Mkurugenzi wa NEMC, Boniventure Baya, alisema kwa sasa wataalamu waliosajiliwa wamefikia 145 na makampuni ya mazingira ni 21.
Alisema kwa sasa mtaalamu ambaye atafanya kazi za kitaalamu bila kuwa na cheti kazi zake hazitopokelewa na baraza lake na kuwataka wataalamu waliosajiliwa kuwa macho na wataaalamu wasio na vyeti.
Chanzo :Ippmedia

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen