Best Blogger TipsSoon

Sonntag, 27. Februar 2011

TZMPAKAAU

Warioba ashauri njia kuelekea shirikisho Afrika Mashariki
Jaji Joseph Warioba amesema kuwa wakati wote ameunga mkono mfumo wa serikali mbili katika muundo wa Muungano na kwamba anatambu mafaniko makubwa ayaliyofikiwa katika Muungano huo.
Jaji Warioba alitoa ufafanuzi huo juzi kwa NIPASHE kufuatia habari iliyomnukuu ikisema kuwa anataka wenye maoni ya kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika mawazo yao yaheshimiwe.
Akizungumza katika mjadala uliowashirikisha wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam waliokutaka kujifunza muundo wa Muungano wa Tanzania katika kufanikisha Shirikisho la Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki, Jaji Warioba alizitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuiga mfano wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuhakikisha Shirikisho la Afrika Masharikli linalopendekezwa kuanzishwa linafanya kazi vizuri.
Jaji Warioba alisema nchi wanachama wa EAC zinapaswa kuwa tayari kuacha mamlaka za nchi zao kama zinataka kufikia kwenye Shirikisho.
Alisema kama nchi hizo hazitakuwa tayari kufanya hivyo zitakuwa zinajigawa kisiasa badala ya kuwa na umoja na kuwaunganisha wananchi wa ukanda huo.
"Ninachokisema ni kwamba vyovyote tutakavyofanya katika nchi zetu, lazima tukumbuke mchakato wa kuelekea katika Shirikisho la Afrika Mashariki," alisema.
Warioba aliwaambia washiriki wa mjadala huo kuwa mafanikio ya Muungano wa Tanzania umekuwa imara ingawa kuna matatizo madogo madogo.
Aliongeza kuwa wananchi wa Tanzania walianza kuwa kitu kimoja tangu mwaka 1960 ingawa wakati fulani kulikuwa na pasi za kusafiria kutoka upande mmoja wa Muungano kwenda mwingine.
Hata hivyo, alisema kuna kazi kubwa ya kufanya katika kufikia haki za raia na za kisiasa, kwa mfano ili mtu aweze kupiga kura Zanzibar kumchagua Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani, anatakiwa kuwa amekaa visiwani hapo kwa muda usiopungua miaka mitatu mfululizo.
"Kwa Mtanzania bara hawezi kupiga kura visiwani kadhalika Mzanzibari ambaye ameishi bara anakosa nafasi hiyo kuwachagua viongozi wao," alisema.
Alisema kwa upande wa Tanzania Bara Watanzania wote wana haki zote za kuchagua na kuchaguliwa bila kujali wanatoka sehemu gani ya Jamhuri. Mzanzibari anaweza kupiga kura na kuomba kuchagauliwa katika Bunge ka Muungano na serikali za mitaa.
Jaji Warioba alisema maoni ya kutaka kuanzishwa kwa serikali ya Bara (Tanganyika) inaweza kuleta madhara kama yale yale ya Zanzibar ya kuvunja haki za wananchi katika kuchagua na kuchaguliwa, hali ambayo ni kurududi nyuma dhidi ya mafanikio yaliofikiwa na itadhoofisha Muungano.
Alisema kuanza kwa mfumo huo kutakuwa na Wabara ambao haki zao za kisiasa na kijamii zimezuiwa Zanzibar na kutakuwa na Wanzanzibari ambao haki hizo zikezuiwa kwa pande zote, yaani Visiwani na Bara.
Tofauti na tulivyoripoti juzi, kwamba Warioba anaunga mkono maoni ya kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika, msimamo wake ni wa kuunga mkono mfumo wa sasa wa serikali mbili ambao umeimarisha Muungano

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen