Best Blogger TipsSoon

Freitag, 18. Mai 2012

TZMPAKAAU

TUKIO ZIMA LA AJALI  YA PATRICK MAFISANGO
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) na timu ya Simba Patrick Mutesa Mafisango (32), amefariki dunia jana alfajiri kwa ajali ya gari.Amepata ajali hiyo akitokea kwenye Ukumbi wa Starehe wa Club Maisha uliyopo Masaki. Akizungumza Dar es Salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu, alisema Mafisango alikubwa na mauti hayo eneo la Keko jirani na Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam.Alisema Mafisango amekufa kwa ajali ya gari, baada ya gari alilokuwa anaendesha kuacha njia na kugonga mti ulio pembezoni mwa barabara ya Chang’ombe majira ya saa kumi kasorobo alfajiri na kufariki papo hapo.

Gari aina ya toyota cresta aliyopata nayo ajali marehemu Patrick Mafisango. 

Kaburu ameongeza gari hilo ndani lilikuwa na abiria wengine wanne, lakini aliyekutwa na mauti baada ya ajali ni Mafisango pekee. Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kusafirishwa kwenda kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako atazikwa.Kaburu alisema ingawa alikuwa na uraia wa Rwanda na akiichezea timu ya taifa ya nchi hiyo (Amavubi), Mafisango alikuwa ni mzaliwa na raia wa DRC na uamuzi wa kuzikiwa huko ni wa familia yake. 
Watu wengi walikuwepo leaders kuuaga mwili wa marehemu  Patrick Mafisango hawa ni makocha wa Taifa stars.
Msiba wa Mafisango uko katika eneo la Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka Mawili eneo la njia Panda ya Sigara.Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa  Ijumaa saa nne asubuhi katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya mwili wakekusafirishwa kwenda Kinshasa majira ya saa kumi jioni.
Vyanzo:TZMPAKAAU , The Habari,Global Publishers na in2eastafrica

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen