Best Blogger TipsSoon

Dienstag, 25. Oktober 2011

TZMPAKAAU

CHADEMA  YAFIKA  NJOMBE NA KUWEKA NGOME
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kuitikisa ngome ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, baada ya kufungua matawi ya chama hicho katika mkoa mpya wa Njombe na kuingiza wanachama wapya zaidi ya 100 ambao ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katibu mkuu wa CHADEMA DK.Wilboard Slaaa
Hatua hiyo ya Chadema imelenga kujiimarisha katika maeneo ya vijijini, ikiwa ni pamoja na kufuta utamaduni wa baadhi ya viongozi wa chama tawala kupita bila kupingwa katika chaguzi mbalimbali.
Chadema kimeingia katika Jimbo la Spika Makinda la Njombe Kusini katika ziara ya viongozi wa chama hicho katika mkoa wa Njombe.
Ndugu.Thomas Nyimbo
Akizungumza jana na wakazi wa Kata ya Mtwango, Tarafa ya Makambako Wilaya ya Njombe, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Njombe Magharibi (sasa mhamasishaji wa Chadema Mkoa wa Njombe), Thomas Nyimbo, alisema tayari amepokea kadi 10,000 kutoka makao makuu ya chama hicho kwa ajili ya kuzigawa kwa wanachama wapya wanaojiunga na Chadema.
Vyanzo:TZMPAKAAU na IPPMEDIA

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen