
Jengo la bunge la Italia
Serikali ya mseto ya Waziri Mkuu Silvio Berlusconi nchini Italia imekubaliana juu ya mapendekezo ya pamoja juu ya kufanya mageuzi ya kiuchumi, wakati umebakia muda mfupi kabla ya mkutano muhimu wa kilele, mjini Brussels, wa viongozi wa Umoja wa Ulaya watakaoujadili mgogoro wa madeni.
Kiongozi wa chama kidogo cha Northern League kilichomo katika serikali hiyo ya mseto, bwana Umberto Bossi amesema mapatano ya muda yamefikiwa.
Hata hivyo serikali ya mseto ya Italia bado imo katika hatari ya kuvunjika hasa kutokana na lengo la Waziri Mkuu Berlusconi la kupandisha umri wa kustaafu hadi miaka 67.
Umoja wa Ulaya umeitaka Italia iwasilishe kwenye mkutano maalumu wa leo mjini Brussels, tamko la maandishi la kukubali kufanya mageuzi katika mfumo wake mbovu wa fedha.
Vyanzo:TZMPAKAAU na DEUTSCHWELLE
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen