Best Blogger TipsSoon

Sonntag, 5. August 2012

TZMPAKAAU

HOFU YA KUVUNJIKA MUUNGANO YATANDA (THE  WORRIES SPREAD CONCERN THE TANZANIAN UNION  )


Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauwezi kuvunjika kwa mjadala wa Katiba mpya unaoendelea kutokana na kulindwa na sheria ya kuuda Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya ya mwaka 2012.
Msimamo huo umeleezwa
na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) walipokuwa wakijadili mada kuhusu sheria ya mabadiliko ya Katiba mpya iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakary Khamis Bakary huko Chukwani Zanzibar jana.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma, (CCM) alisema kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 9(1) cha sheria ya mabadiliko ya Katiba Muungano umewekewa kinga ya kutovunjika kupitia majadala wa Katiba mpya ya muungano unaoendelea Zanzibar na Tanzania bara.
Alisema kwamba sheria imesema wazi kuwepo kwa Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bunge na Mahakama ni mambo ambayo hayahitajiki kujadiliwa uwepo wake katika utoaji wa maoni ya katiba mpya ya Tanzania.
Hamza alisema kwamba Muungano utaendelea kuwepo hasa kwa kuzingatia hata viongozi wanne wa kitaifa wamekula kiapocha kulinda na kutetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Alisema viongozi waliokula kiapo kwa mujibu wa katiba ya muungano ya mwaka 1977 ni Rais Jakaya Kikwete, rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais Dk Mohamed Ghalib Bilal na Waziri Mkuu Tanzania Mizengo Pinda.
Aidha alisema viongozi na wananchi lazima waelewe wanapozungumzia kero za muungano malengo yao siyo kuvunja muungano huo isipokuwa ni kuona kero zinaondolewa kwa maslahi ya pande mbili za muungano huo.
Upande wake Mwakilishi Jimbo la Ole (CUF) Hamad Masoud Hamad, alisema kwamba sio kama wanataka muungano uvunjike lakini lazima kufanyike mabadiliko ya katiba yatakayosaidia kuondoa malalamiko ya pande mbili za muungano huo.
Alisema kwamba mfumo wa sasa wa Muungano unainyima Zanzibar fursa mbali mbali kama nchi za kuweza kujiamlia mambo yake ya kiuchumi na ushirikiano wa kimataifa na kutaka kuangaliwa upya kwa tatizo hilo.
Alisema kwamba jambo la msingi kwa Wazanzibari ni kuondoa hofu na kuwa kitu kimoja katika kutetea maslahi ya Zanzibar wakati huu wa mjadala wa katiba mpya ya Tanzania.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu,(CUF) alisema kwamba mfumo wa sasa wa muungano haufai na kutetea mfumo wa muungano wa mkataba kama unaotumiwa na muungano wa Jumuiya ya Ulaya (EU).
Naye Waziri wa Afya Juma Duni Haji alisema kwamba Zanzibar ilipoteza nguvu za kutetea maslahi yake ndani ya Muungano baada ya kukubali kunganisha kwa chama cha Afro Shirazy Part na TANU mwaka 1977.
Mwakilishi wa Jimbo la kiwani Hija Hassan Hija (CUF) alisema kwamba Tume ya kuratibu maoni ya Katiba imeanza kazi vibaya Kisiwani Pemba.
Alisema kwamba wananchi wamekuwa hawapewi taarifa za maeneo yanayofanyika mikutano pamoja na muda wa mikutano hiyo na (masheha) na wakuu wa Wilaya na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Mohamed Haji Khalid wa Jimbo la Mtambile (CUF) alisema Uhuru wa Zanzibar wa mwaka 1963 haukuwa bandia kama ilivyoelezwa na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Abubakary Khamis Bakary.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen