HATIMA YA MADAKTARI KUJULIKANA KESHO
Serikali imesema madai ya madaktari ya kutaka kuongezewa maslahi yatatolewa maamuzi kesho baada ya suala hilo kuwa kwenye majadiliano.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii, Dk. Hussen Mwinyi, alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa suala hilo kwa kuwa bado liko kwenye mazungumzo na kuahidi kulitolea taarifa kesho.
"Nikizungumzia kwa sasa nitakuwa nimeingilia mazungumzo ambayo yanaendelea hivyo nipe muda kidogo mpaka Jumatatu nitatoa taarifa dhidi ya suala hilo," alisema Dk. Mwinyi
Wiki iliyopita madaktari waliipa serikali muda wa wiki mbili kuhakikisha inatimiza madai yao na kama itashindwa kufanya hivyo wataandaa mgomo nchi nzima.
Pia madaktari hao wamepinga vikali kuipokea ripoti ya kamati ya serikali ambayo ilipewa kazi ya kushughulikia sakata la madaktari.
Walieleza kuwa taarifa ya kamati hiyo imeshindwa kueleza jinsi gani itashughulikia madai yao ikiwemo suala la nyongeza ya mshahara ambapo walitaka iwe sh milion 3.5 kwa kima cha chini.
Vyanzo:TZMPAKAAU na Ippmedia
Vyanzo:TZMPAKAAU na Ippmedia
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen