Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 3. Mai 2012

TZMPAKAAU

WENGI WAZIDI KUIHAMA CCM
MZIMU wa CCM kukimbiwa na wanachama wake na kujiunga na CHADEMA umeendelea baada ya wanachama 70 kukihama chama hicho.Wanachama waliohama chama hicho ni wa Kata ya Endulen iliyopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. 
Pichani kulia ni Mch Israel Natse Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya CHADEMA
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mbunge wa Jimbo la Karatu, Bw.Izrael Natse jana aliwataka viongozi wa CCM kuacha kuwatisha wananchi wanaohama na kujiunga na CHADEMA.Bw.Natse alisema CHADEMA ni chama pekee cha kisiasa nchini kilicho na malengo ya kweli ya kuwaletea mabadiliko Watanzania na ndiyo maana kimekuwa kikikubalika na kuaminiwa na wananchi kwa kasi ya aina yake.Aliwahimiza wananchi wa Kata Endulen wilayani Ngorongoro, ambapo ndipo ngome ya CCM kuacha uoga na kujitokeza kwa wingi kurudisha kadi za CCM  na kujiunga na CHADEMA.
Vyanzo:TZMPAKAAU na Majira

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen