Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 18. April 2012

TZMPAKAAU

UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI UNA KASORO:KAMBI YA UPINZANI
Freeman Mbowe mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni.

Wakati Bunge likitarajia kufanya uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kesho, Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, imetishia kwenda Mahakama ya Afrika Mashariki kama kanuni na taratibu za uchaguzi huo hazitafuatwa.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kutoka Dodoma jana, Kiongozi wa Kambi hiyo, Freeman Mbowe, alisema tayari kambi hiyo imewasilisha malalamiko ya dosari kwenye uchaguzi huo kwa Katibu wa Bunge; ikipendekeza kwamba kanuni zirekebishwe ili kutoa viti zaidi vya wabunge kwa vyama vya upinzani badala ya kiti kimoja kinachotolewa hivi sasa.
Alisema: “Sisi tunaona kwamba uchaguzi unapelekwa sivyo, unafanyika kimakosa kwa sababu haiwezekani vyama vyote vya upinzani vyenye wabunge na visivyo na wabunge, vikapewa kiti kimoja; tunapendekeza angalau viwe vitatu au vikipungua kabisa viwe viwili.”
Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kupewa viti vinane kwenye Bunge hilo ni upendeleo ambao unaweza kuwavuruga Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, alisema anaamini kwamba suala hilo litatazamwa na kufanyiwa kazi na ofisi ya Bunge kabla ya uchaguzi huo ili Watanzania wapate haki ya kuwakilishwa kikamilifu kwenye chombo hicho.
Vyanzo:TZMPAKAAU na The habari


Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen