Best Blogger TipsSoon

Montag, 9. April 2012

TZMPAKAAU

TAMASHA LA MUZIKI WA INJILI LAFANA

Kulia ni waziri wa Mambo ya Nje Bebard Membe akiangalia album inayoitwa utukufu wa Mungu kutoka kwa Solomon Mukubwa aliye katikati,kulia ni mwandaaji wa Tamasha hilo Bw. Msama ambaye pia ni mkurugenzi wa Msama Promotions.
Kulia ni Msama,Katikati ni Bw.Benard Membe akimsalimia mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya Emi Kosgei kushoto.
Rebecca Malope alipamba Tamasha hilo kwa staili yake ya kipekee ya kumsifu Mungu,Rebecca Malope ni mwimbaji maarufu wa Nyimbo za injili nchini Afrika Kusini.
Hapa  Rebecca Malope mwenye mic akiwa pamoja na Rose Mhando jana uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Rose Mhando ambaye aliwaahidi mashabiki wake kumuinua Yesu siku hiyo alikuwa akifanya mambo stejini.
Rose Mhando akiwaimbisha mashabiki wa mziki wa Injili.
Hapa ni Upendo Kilahiro maarufu kwa kibao chake cha "Unajibu Maombi" naye akitumbuiza kwa jina la Yesu.

John Lissu naye alikuwepo John Lissu ni mwimbaji maarufu katika mziki wa Injili  Live hapa akiwa na kikundi chake.


Benard Membe aliyasema haya katika tamasha hilo,kwamba vitendo vya kifisadi na kuporomoka kwa maadili katika jamii ni vitu visivyohitaji kuvumilika katika jamii ya watanzania, zaidi ya hayo mheshimiwa Bernard Membe akizungumzia suala la katiba mpya, amewahamasisha wananchi kutoa maoni yao na kupendekeza katiba wanayoitaka kadhalika Bernard Membe alisema wapo watu watakaotumia fursa hiyo kutaka kupandikiza chuki na ametahadharisha kuwaepuka watu wa aina hiyo.Pamoja na hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw.Bernard Membe alielezea kusikitishwa na kifo cha msanii maarufu wa Filamu za Kitanzania Steven Kanumba na kuongeza kuwa Kanumba alikuwa balozi wa Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia filamu alizokuwa akizicheza.


Vyanzo:TZMPAKAAU,Mjengwa,Michuzi na FullShangwe 

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen