Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, na wahariri wa vyombo vya habari, wameazimia kutekeleza mambo makuu manne ili kukidhi mahitaji ya wadau hao ya kudumishwa kwa amani, usalama na utulivu nchini.Kwa mujibu wa taarifa ya maazimio hayo, azimio la kwanza ni wadau hao kuwa na msukumo wa pamoja katika kuandaa ajenda mbalimbali zitakazoielimisha, kuihamasisha na kushawishi jamii katika kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu nchini. Taarifa hiyo ilitaja azimio la pili kwamba, ni wadau hao kuwa daraja kati ya wananchi na Jeshi la Polisi.
Hilo ni kwa kutumia vyombo vinavyoongozwa na jeshi hilo katika kuhakikisha kuwa jamii inapata na kufahamu taarifa na habari zitakazosaidia kubaini na kuzuia vyanzo vya uhalifu.
Azimio la tatu ni kuandaa ziara za kimafunzo ili wadau wa habari kuweza kujifunza na kuona namna maboresho ya jeshi hilo yanayofanyika kwa vitendo na hatimaye kuwa na mtazamo wa pmoja katika kuihabarisha jamii. Taarifa hiyo ilitaja azimio la nne na la mwisho kuwa ni pande mbili hizo kukutana kila baada ya miezi mitatu.
Vyanzo:TZMPAKAAU na Ippmedia.
Vyanzo:TZMPAKAAU na Ippmedia.
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen