(RESIGNATION OF MINISTER HADJI MPONDA STILL DOUBTFUL)
Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii Dk.Hadji Mponda.
(Minister of Health and Social Welfare Dk.Hadji Mponda)
Hatma ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, ambaye anashinikizwa ajiuzulu kutokana na kuboronga mambo katika kushughulikia mgomo wa madaktari, bado ni kitendawili.(Minister of Health and Social Welfare Dk.Hadji Mponda)

Katibu Mkuu wa Ikulu, Peter Alanambula Ilomo, alisema suala la kuchukuliwa hatua za kuwajibishwa Dk. Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, kutokana na mgomo wa madaktari, lipo juu ya uwezo wake hivyo hawezi kulitolea maelezo kama Rais Jakaya Kikwete amechukua uamuzi gani hadi sasa dhidi ya viongozi hao.
“Mimi ni Katibu Mkuu Ikulu, lakini katika suala la Waziri wa Afya na Naibu wake, angeulizwa Katibu Mkuu Kiongozi, yeye ndiye anaweza kujua kama Mheshimiwa Rais amechukua hatua gani".
Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia na Swahilivilla
Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia na Swahilivilla
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen