Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 29. Februar 2012

TZMPAKAAU

 Rais.Kikwete alihusika:Costa Mahalu
If Scam?,it had Kikwete blessings:Costa Mahalu
ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Jakaya Kikwete alitia saini kuidhinisha bei ya jengo la ubalozi wa Tanzania huko Italia hivyo kumpa nguvu ya kisheria ya uwakilishi katika ununuzi wake.
Mahalu alidai mahakamani hapo jana kuwa Kikwete alikubali bei ya Euro 3,098,741.58 kwa ajili ya ununuzi wa jengo hilo na alitetea uamuzi wake huo alipoliambia Bunge Agosti 3, 2004.
“Wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha 39 kilichofanyika Agosti 3, 2004, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Jakaya Kikwete alithibitisha kuwa jengo hilo liligharimu Euro 3,098,741.58 kwa kuanzia,” alisema Mahalu na kuendelea:
Kulia ni aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italy Costa Mahalu.

“Mheshimiwa hili linaweza kuthibitika ukisoma kumbukumbu za Bunge za Kitabu cha mwaka 2004 ukurasa wa 169 aya ya pili. Mwaka 2001/2002 Wizara ilinunua jengo Roma kuondokana na adha ya kupanga nyumba za watu na kulipa kila mwaka. Wizara ya Ujenzi kila mwezi. Machi 16, 2002 ilitoa hundi ya kwanza ya Euro700 milioni kati ya Euro 3,098,741.58,” alisema.
Profesa Mahalu ambaye alitinga mahakamani huku akiwa na  kabrasha kubwa la vielelezo, aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta wakati akiendelea kutoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60.
Soma zaidi: http://www.mwananchi.co.tz/mwananchi-jumapili/37-tanzania-top-news-story/20644-balozi-mahalu-amlipua-jk-mahakamani.html
Vyanzo:TZMPAKAAU,Mwananchi na Ippmedia.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen