Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 9. Februar 2012

TZMPAKAAU

 WAZIRI MKUU AKUTANA NA MADAKTARI  LEO,AMFUTA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA BI. BLANDINA NYONI  NA MGANGA MKUU WA SERIKALI
Waziri mkuu alipokuwa akiongea na madaktari katika hospitali ya taifa ya  Muhimbili Dar es salaam.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na madaktari  leo katika hospitali ya taifa Muhimbili,ametangaza kumfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya afya bi Blandina Nyoni na mganga mkuu wa serikali bw. Deo Mutasiwa.Vigogo hao wamefutwa kazi kutokana na kuonekana kama kiini cha mgogoro .Mgogoro uliopelekea madaktari kugoma katika nchi nzima kwa takriban wiki mbili na kuwaacha wagonjwa wengi wakipoteza maisha na wengine hali zao ziekindelea kudhoofika.

Kushoto ni Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma Bi.Hawa Ghasia katikati ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Muhimbili Bi.Marina Njekela.


Katika hatua nyengine waziri mkuu amewataka madaktari kuunda tume yao wao wenyewe itakayokusanya madai ya madaktari w(y)ote na kumpelekea madai hayo ili aweze kuyashughulikia.
Mmoja wa  madaktari akieleza jambo katika kikao  hicho.
Mwisho waziri mkuu amewataka madaktari hao kurejea kazini ili kuokoa maisha ya watanzania.
TZMPAKAAU inawapa pole wale wote wanaougua na wanaouguliwa katika kipindi hichi kigumu....na TZMPAKAAU inaitaka serikali na madaktari kuutatua mgogoro huu mapema iwezekanavyo kuepusha madhara makubwa zaidi.
Vyanzo:TZMPAKAAU na MICHUZI.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen