Best Blogger TipsSoon

Sonntag, 15. Januar 2012

TZMPAKAAU

Regia Mtema afariki dunia

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema, amefariki dunia jana majira ya saa 5:15 baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika eneo la Ruvu JKT, mkoani Pwani.
Taarifa fupi ya Spika Makinda iliyotolewa Dar es Salaam jana ilieleza kwamba taarifa kamili juu ya msiba huo itatolewa baada ya ofisi ya Bunge kuwasiliana na familia ya marehemu.


“Kwa masikitiko makubwa nawatangazia waheshimiwa wabunge na wananchi wote kwamba Mhe. Mtema amefariki dunia kwa ajali ya gari leo eneo la Ruvu, mkoani Pwani…Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,” alisema Makinda katika tangazo hilo.
CHADEMA YASIKITISHWA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo na kutoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wote wa Mbunge huyo.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika, alisema marehemu alikitumikia chama kwa uadilifu na alijituma katika kila suala linalohusu chama chake.
Gari iliyoondoka na mbunge Regia
CUF WATOA POLE
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, alisema katika taarifa yake jana kuwa anaamini kwamba Watanzania, hasa wapinzani wamepoteza kijana mahiri na mpambanaji kwa ajili ya Tanzania iliyo bora.
“CUF tumekuwa tukimwona marehemu Regia Mtema kama mbunge jasiri miongoni mwa wabunge wanawake aliyekuwa akileta changamoto kwa watawala wa Tanzania kutokana na michango yake bungeni na nje ya Bunge,” alisema Mtatiro.
Vyanzo:Ippmedia,TZMPAKAAU,Mtaa kwa Mtaa na Haki ngowi

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen