Zaidi ya Shilingi milioni 125 zilipatikana katika harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kidingo mkoani Kigoma iliyoendesha na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Lowassa na marafiki zake walichangia Sh. nilioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo iliyoko Kata ya Mwandiga wilayani Kigoma.

Akizungumza katika hafla hiyo, Lowassa alisema kuna vijana wengi waliokosa ajira, ambao alisema ni bomu linalosubiri kulipuka. Alisema vijana wengi wanamali za shule na vyuo, lakini wanakosa ajira.
Aliiomba serikali na wadau mbalimbali nchini kukaa chini kupanga mikakati ya namna ya kuwasidia wapate ajira.
Aidha, aliwataka watu waliomali za masomo wasisubiri ajira za serikali badala yake wajiunge katika vyuo vya ufundi stadi ili wajiajiri.
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen