Best Blogger TipsSoon

Samstag, 3. Dezember 2011

TZMPAKAAU

Baada ya dhiki faraja:Jerry Muro sasa mambo safi
Jerry Muro aliyekuwa mwandishi wa ITV na baadaye mwandishi maarufu wa  TBC katika kipindi chake  cha usiku wa habari,kipindi kilichojizolea umaarufu kwa kuibua maovu na uozo mbalimbali uliokuwa ukitokea hasa katika sekta za umma.Lakini Jerry alishtakiwa mwezi februari mwaka jana akikabiliwa na tuhuma za kuomba rushwa...tuhuma zilizompotezea umaarufu wake,na hata kazi yake kama mwandishi...mwishoni akijikuta akiranda randa mitaani.Baada ya dhiki faraja.
                                 Jerry C. Muro.
Wiki iliyopita Jerry Muro alipata mwenzi wa maisha Jennifer John,Na walifunga ndoa katika kanisa la Lutheran la Azania Front ndoa iliyofana sana kwa kuhudhuriwa na wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi.
Hapa ni aliyekuwa mwandishi wa TBC Jerry Muro na mwenzi wake Jennifer John.
Mambo yalikuwa hivi siku ya harusi yao wiki iliyopita, Jerry alikula kiapo: “Mimi Jerry Muro, nakubali Jennifer John awe mke wangu, katika shida na raha, katika dhiki na faraja, nimpende na kumtunza hadi kifo kitakapotutenganisha…”
Ilipofika zamu ya Jennifer, alifunguka: “Mimi Jennifer John, nakubali Jerry Muro awe mume wangu, katika shida na raha, katika dhiki na faraja, nimpende na kumtunza hadi kifo kitakapotutenganisha…”Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ‘babkubwa’ iliyofanyika katika Ukumbi wa Kramuu uliopo Mbezi Tangibovu, Dar ambapo watu walikula na kunywa hadi wakasaza.


Jerry Muro na wakili wake bw Majura Magafu


Jerry Muro alishinda kesi iliyokuwa inamkabili siku ya Alhamisi . Mahakama ya kisutu mbo yalikuwa hivi siku Jerry alipofutiwa mashtaka na kuachiwa huru .
Jerry alipokuwa akiingia mahakamani na mke wake siku ya Alhamisi
Frank Moshi hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu alimwachia huru Jerry  huru baada ya mahakama hiyo kubaini mapungufu yalikuwemo upande wa mashitaka kwenye mwenendo mzima wa kesi hiyo. Akikubaliana na hoja za upande wa utetezi, aliwaachilia huru pia wenzake wawili ambao ni Edmund Kapama na Deogratius Mgasa.
Jerry Murro atunukiwa zawadi ya mwandishi bora
Mambo yamezidi kumyookea Jerry baada ya kukabidhiwa zawadi kama mwandishi bora wa habari za kiuchunguzi mwaka 2009.Baraza la habari Tanzania (MCT) lilimkabidhi  Jerry hundi ya dola 4000 jana kwa kutambua mchango wake katika kutoa habari za kiuchunguzi akiongea Jerry kwa upande wake , Muro amewataka waaandishi wa habari kujikita zaidi katika habari za uchunguzi kwani changamoto ni kubwa na wanahitaji kufanya kazi kwa kujitolea na wachukue mfano wake kama kichocheo cha kusonga mbele na si kurudi nyuma.
Vyanzo:TZMPAKAAU na IPPMEDIA


Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen