Best Blogger TipsSoon

Samstag, 26. November 2011

TZMPAKAAU

SASA NI ZAMU YA MCHUNGAJI
(A PASTOR  DETAINED BY MOSHI POLICE BECAUSE HE INVITED OPPOSITION LEADER TO A CHRISTIAN CONFERENCE)

  • Ashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumwalika Philemon Ndesamburo
                            Philemon Ndesamburo opposition member of parliament invited
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limemshikilia kwa saa kadhaa mchungaji wa Kanisa la Agape kituo cha Moshi, David Mushi, kwa kilichodaiwa kuendesha mkutano wa wa injili ambao una itikadi za kisiasa.


Mchungaji huyo alikamatwa muda mfupi baada ya Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo, kumaliza kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo katika viwanja vya Mashujaa juzi ambapo Kamanda wa Polisi Wilaya ya Moshi, Silvanus Rukaga, alifika na kumkamata.

Inadaiwa na waumini hao kuwa, katika ufunguzi huo walimualika Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, ambaye alitoa udhuru  na kumwagiza mwakilishi wake ambaye pia hakufika ndipo walipoamua kumualika Ndesamburo, ambaye alikubali mwaliko wao.
                      Mchungaji Venon Fredinandes
Taarifa za ndani zinabainisha kuwa katika mahubiri yake, Mkurugenzi wa kituo cha televisheni cha Agape, Venon Fernandus, alipinga vikali kuwa mkutano wao ulikuwa wa kisiasa na kusema kuwa maudhui ya mkutano huo ni kuliombea Taifa.
Mmoja kati ya Muumini ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, aliliambia NIPASHE kuwa baada ya Ndesamburo kuufungua, walishangaa kuona gari la Rukaga kufika viwanjani hapo na kumchukua mchungaji wao na kuondoka naye.
Alisema mara baada ya kuondoka naye zililetwa taarifa kuwa mchungaji huyo, David Mushi, anahojiwa kutokana na kuendesha mkutano wenye maudhui ya kisiasa tofauti na kibali walichopatiwa, jambo ambalo walitakiwa kupeleka ushahidi.
Baada ya mchungaji huyo kuhojiwa, alitakiwa kuwasilisha mkanda wa video  wenye mahubiri yake pamoja na hotuba ya mbuge huyo ili waweze kuutazama jambo ambalo walifanya.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Absolum Mwakyoma alipofuatwa na kuulizwa kuhusu jambo hilo hakupatikana kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa nje ya ofisi kikazi na alipopigiwa simu yake ya mkononi,  alisema hana taarifa hizo na kama jambo hilo lipo ataletewa na atatoa taarifa.
Vyanzo:TZMPAKAAU na IPPMEDIA

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen