DENMARK KUPATA WAZIRI MKUU WA KWANZA WA KIKE
Chama cha Social Demokrat na vyama shirika vinaongoza kwa wingi mdogo, baada ya takriban kura zote kuhesabiwa katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hapo jana nchini Denmark.

Ionekanavyo, mwenyekeiti wa chama cha Social Demokrat, Helle Thorning-Schmidt atakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa waziri mkuu nchini Denmark. Thorning- Schmidt amejitangaza mshindi wa uchaguzi huo.
Waziri Mkuu wa sasa, Lars Leokke Rasmussen amekiri kuwa ameshindwa na amesema baraza la mawaziri litavunjwa. Chama cha Kiliberali cha Rasmsussen kinachoelemea mrengo wa kulia na chama cha wahafidhina vilitawala Denmark kwa takriban miaka kumi kwa wingi mdogo na kimeungwa mkono bungeni na Chama cha Umma chenye sera kali za mrengo wa kulia. Chama hicho kimeshinikiza sera kali za kudhibiti uhamiaji.
Vyanzo:TZMPAKAAU,DEUTSCHWELLE
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen